Kutuhusu

Idara ya Msaada wa Uendeshaji (DOS) hutoa msaada wa uendeshaji kwa idara za Ukatibu wa Umoja wa Mataifa duniani kote, ikiwa ni pamoja na huduma za ushauri, uendeshaji na usaidizi wa shughuli. Ofisi ya Shughuli za Msaada (OSO) ni mojawapo ya nguzo za idara ya DOS. Inatoa huduma maalum za ushauri, uendeshaji, na msaada wa shughuli kwa zaidi ya idara 100 za Ukatibu wa Umoja wa Mataifa duniani kote. Msaidizi wa Katibu Mkuu OSO inasimamia nguzo tatu: Huduma za Rasilimali Watu, Usimamizi wa Huduma ya Afya na Usalama na Afya Kazini, na Ukuzaji wa Uwezo na Mafunzo ya Uendeshaji.

Taarifa ya Dhamira ya Kitengo cha Usimamizi wa Huduma ya Afya na Usalama na Afya Kazini (DHMOSH) 

DHMOSH chini ya ofisi ya OSO inalenga kulinda na kukuza afya ya wafanyakazi, kudumisha na kuboresha uwezo wao wa kufanya kazi, kuchangia katika mazingira salama na yenye afya ya kufanya kazi, na kukuza urekebishaji wa kazi kulingana na uwezo wa wafanyakazi, kwa kuzingatia hali ya afya zao.

Kitengo cha DHMOSH kinakuza na kuliganisha shughuli zake kulingana na vipaumbele vya kimkakati vya shirika, kikilenga haswa mifumo ya usimamizi inayohitajika kushughulikia mahitaji ya kimfumo ya matibabu, usalama na matibabu ya kazini yanayohusiana na ongezeko la uwepo wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa duniani kote.

Mkakati wa Afya ya Akili kwa Wahudumu Wasio wa Usalama ni mojawapo ya kipaumbele kama hicho. Kupitia utekelezaji na uanzishaji wake wa Mifumo ya Dijitali ya afya ya akili, kitengo cha DHMOSH kinalenga kufanya usaidizi wa afya ya akili uweze kufikiwa, kupunguza vizuizi vya kutafuta usaidizi, na kupunguza unyanyapaa kuhusu masuala ya afya ya akili miongoni mwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaovaa sare.